Mfuko wa dhamana wa North Mara ni matokeo ya mgongano wa kimaslahi baina ya Keng’anya Enterprises Limited (KEL) yenye hati usajili namba 17118 na Placer Dome (T) Limited (PDT) yenye hati ya usajili namba 23446 (awali ilijulikana kama Afrika Mashariki Gold Mines Limited na sasa ni African Barrick Gold). Mgongano huu unarejea shauri nambari 298 ya mwaka 1997 na 315 ya mwaka 2002 yaliyoamuliwa nje ya mahakama na kusajiliwa mahakama kuu ya Tanzania, mnamo mwezi Desemba 2004.
KEL na PDT pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Dhamana uliotarajiwa kuanza Januari 2006 kwa ajili ya kusaidia vijiji vitano vya Kerende, Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja vilivyo na mkataba na mgodi wa North Mara.
Previous
Next
Wachangiaji pekee katika huu mfuko (wafadhili) hadi sasa ni wawili tu; NORTH MARA GOLD MINES (NMGM) pamoja na KENG’ANYA ENTERPRISES (KEL). Vijiji havijawahi kuchangia huu mfuko na wala hakuna kiasi chochote cha fedha zitokanazo na mrahaba wa vijiji zilizowahi kuingizwa na mgodi katika mfuko huu.
Wanufaikaji wa mfuko huu ni vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa North Mara, ambavyo ni; Nyangoto, Kewanja, Genkuru, Nyamwa-ga na Kerende.