Picha ya pamoja kati ya Meneja wa mfuko wa dhamana, Wafanyakazi wa mfuko wa Dhamana, Diwani wa Kata ya Nyamwaga (Waliosimama Juu) na (Waliosimama Chini) ni Wakuu wa Shule za sekondari zinazozunguka Mgodi wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi Zawadi kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne waliopata Division One kwenye mitihani ya NECTA 2021.
Hafla ya kuwazawadia wanafunzi vinara wa NECTA 2021
Trustee Arphaxard E. Chacha (wa kwanza kushoto) na Trustee Peter Msabi (wa pili kulia) akiwa na wajumbe wa Kamati tendaji kutoka Vijiji vya Nyamwaga na Genkuru.
Ushiriki katika masuala ya jamii
Meneja wa Mfuko wa Dhamana Mr. John Waigama akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga mwenye shati la Kitenge, Afisa Mahusiano wa Acacia North Mara, Richard Ojendo (wa kwanza kushoto) pamoja na General Manager wa Acacia North Mara walipotembelea Banda la mfuko wa Dhamana kwenye Maonesho ya Mahusiano na Acacia North Mara yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ingwe Sekondari mwaka 2017.
Maonesho ya Mahusiano na Acacia North Mara
Mfuko wa dhamana wa North Mara ni matokeo ya mgongano wa kimaslahi baina ya Keng’anya Enterprises Limited (KEL) yenye hati usajili namba 17118 na Placer Dome (T) Limited (PDT) yenye hati ya usajili namba 23446 (awali ilijulikana kama Afrika Mashariki Gold Mines Limited na sasa ni African Barrick Gold). Mgongano huu unarejea shauri nambari 298 ya mwaka 1997 na 315 ya mwaka 2002 yaliyoamuliwa nje ya mahakama na kusajiliwa mahakama kuu ya Tanzania, mnamo mwezi Desemba 2004. KEL na PDT pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Dhamana uliotarajiwa kuanza Januari 2006 kwa ajili ya kusaidia vijiji vitano vya Kerende, Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja vilivyo na mkataba na mgodi wa North Mara
Wazo kuu lililopelekea kuundwa Mfuko lilitokana na ukweli kwamba, baada ya Maisha ya Mgodi kwisha, kuwe na chombo mbadala kitakacholeta chachu ya maendeleo na uwepo wa maisha kiuchumi (livelihood). Hivyo basi Mfuko ukaanzishwa ili uwe chombo endelevu kitakachosaidia kutoa huduma mbalimbali za kijamii, na kuchangia maendeleo ya jamii, hasa pale Maisha ya Mgodi yatakapokuwa yamefikia ukomo.
Mfuko wa Dhamana una jukumu la kuhamasisha, kusaidia na kutoa msukumo kwenye miradi na shughuli katika nyanja za elimu, mafunzo, afya, kujenga uwezo, kilimo, maji na kuondoa umaskini kwa kadri wadhamini watakavyoona inafaa.